Baba yangu aliuawa mbele ya macho yangu-Bonfils Nikiza asimulia

Mwanamziki wa nyimbo za injili wa  nchini Burundi Bonfil Nikiza alisimulia vile maisha yamekua magumu kwake alipowasili nchini Kenya, hii ni baada ya babake mzazi kuuwawa mbele ya macho yake.

Katika mahojiano kwenye kituo kimoja cha televisheni nchini mwanamziki huyo aliwaacha wengi machozi yakiwalenga machoni.

Nikiza aliwahadithia Kambua na mwenzake DJ Ken vile familia yake iliuawa nchini Burundi katika mapigano ya kikabila na kubaki peke yake bila msaidizi.

"Nilikuja Kenya kutoka Burundi kwa sababu kulikua na vita nyumbani, baada ya kumaliza kidato cha nne nilifadhaika sana kwa hasara ambayo ilitokea,Nilipoteza familia yangu katika vita hivyo.

Nilijaribu juu chini kupata ajira lakini ilikuwa vigumu kwangu na nikaamua kuondoka Burundi." Alisimulia Bonfils.

Bonfils ameanzisha kampuni yake ya kuwasaidia mayatima, wajane na hata watoto wa mitaa. Alisema sababu kuu ilikuwa kuwasaidia wasiojiweza na kuwaonyesha upendo waliokataliwa.

"Nilipoteza familia yangu nilipokuwa mtoto mdogo, baba yangu mzazi aliuawa mbele ya macho yangu, kwa hivyo najua uchungu wa kumpoteza mmoja wa wapendwa wako.

Niliamua kufanya na kuwasaidia watoto kwa maana na jua uchungu mtu anaopitia." Alisema.

Alisimulia vile ilivyo mchukuwa muda kufika Nairobi ambapo hakuwa anajua mtu yeyote.

"Sikua na pesa za nauli ya ndege, nilipanda lori kutoka burundi ilichukua muda wa wiki mbili kufika Nairobi.

Sikujua mtu hata mmoja Nairobi." Alisema Bonfils.

Bonfils ameimba wimbo 'Tegemeo' akimshirikisha Kambua.