Babu Owino acharuka kuhusu ukosefu wa ajira nchini

Kufuatia kisa cha mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi aliyefuzu na daraja la kwanza mwaka uliopita na bado hajapata ajira kuripotiwa na kituo cha citizen, mbunge wa Embakasi ameicharukia serikali kwa ahadi zake hewa huku akiwaita wanafunzi wote waliofuzu vyuo vikuu kwenye mkutano ili waweze kujua jinsi watakavyo jiokoa kutokana na janga la umaskini.

Kwenye barua yake aliyoweka kwenye mtandao wa kijamii wa instagram, Babu Owino ameelezea dhiki aliyo nayo moyoni mwake kwa vijana wanaomaliza chuo kikuu kwa sasa huku akiwakashifu wazee waliokatalia kazini ama walioa kata kustaafu.

Kwenye barua yake aliyoweka kwenye mtandao wa kijamii wa instagram, Babu owino ameelezea dhiki aliyo nayo moyoni mwake kwa vijana wanaomaliza chuo kikuu kwa sasa huku aki wakashifu wazee waliokatalia kazini ama walioa kataa kustaafu.

'They have done everything they are supposed to do. They have worked hard against difficult challenges to achieve what their leaders told them they needed. Then after all that, they end up in slums while civil servants who have far exceeded the retirement age of 60 continue being shortlisted for government opportunities."

 Babu Owino ameiomba serikali kurejelea maagizo yake aliyekuwa inspecta generali wa polisi bwana Daudi Tonje.

'Tonje Rules' zilisema kuwa iwapo mtu amekaa ofisini ama katika nafasi flani kwa muda flani basi yeye alipaswa kupandishwa cheo au astaafu kulingana na miaka yake.Kwenye sheria zake Tonje, hakuna mtu aliyekuw na ruhusa ya kuishi ofisini zaidi ya muda flani. Sheria hizi zilihakikisha haki na usawa kwa wananchi wote katika utaftaji wa kazi.

Babu amewahidi wanafunzi wote waliofuzu kuwa atawaita mkutano hivi karibu ili kujadiliana hatma ya maisha yao ya baadaye katika uga wa uhuru park.