'Babu Owino alibishana na DJ Evolve kabla ya kumpiga risasi,' - Polisi

DJ babu owino
DJ babu owino
Polisi kutoka kituo cha Kilimani asubuhi ya leo wametoa ripoti kuhusu kisa cha Babu Owino kumpiga risasi jamaa mmoja katika eneo la burudani la B Club lililoko Kilimani.

Katika taarifa yao, walifichua kuwa tukio hilo liliripotiwa saa moja asubuhi Januari 17, 2020 na mkuu wa usalama wa B Club, George Otieno.

Kulingana na bwana Otieno, mbunge huyo wa Embakasi mashariki, Paul Ongili almaarufu Babu Owino, alikuwa kwenye klabu hiyo na kulizuka ubishi baina yake na DJ kwa jina Felix Orinda al maarufu Dj Evolve.

Hapo ndipo Owino alipotoa bunduki yake aina ya pistol na kumpiga Felix risasi ya shingo. Mwathiriwa alikimbizwa na wakuu wa klabu hiyo hospitali ya Nairobi akiwa katika hali mbaya.

Hapo ndipo polisi kutoka Kilimani walidhuru klabu hiyo kabla ya kumkamata mbunge huyo ambaye hivi sasa amezuiliwa katika kituo cha Kilimani.

Polisi walitangaza kuwa hakuna bunduki au mabaki ya risasi yaliyopatikana, ila polisi bado wako kwenye eneo la tukio wakiendeleza uchunguzi wao.

Soma taarifa hiyo,

KILIMANI SUBCOUNTY

KILIMANI POLICE STATION

SUBJECT: SHOOTING INCIDENT REPORT AT B CLUB GALANA PLAZA KILIMANI

IT WAS REPORTED BY ONE GEORGE OTIENO A SECURITY MANAGER AT B CLUB LOCATED ALONG GALANA ROAD WITHIN KILIMANI THAT TODAY 17TH DAY OF JANUARY, 2020 AT AROUND 7:00AM HON. PAUL ONGILI BABU OWINO MEMBER OF PARLIAMENT FOR EMBAKASI EAST WAS IN THE CLUB WHEN HE ARGUED WITH THE DJ OF THE CLUB NAMELY FELIX ORINDA. HE THEN DREW HIS PISTOL AND SHOT THE DJ ON THE NECK. THE VICTIM WAS RUSHED TO NAIROBI HOSPITAL IN SERIOUS CONDITION BY THE MANAGEMENT OF THE CLUB. SCCIO KILIMANI AND TEAM VISITED THE SCENE AND LATER PROCEEDED TO NAIROBI HOSPITAL AND ARRESTED THE MP WHO IS CURRENTLY AT KILIMANI POLICE STATION. NO RECOVERY OF THE FIREARM OR THE CARTRIDGE. OFFICERS CURRENTLY AT THE SCENE SEARCHING FOR THE CARTRIDGE. THE SCENE WAS PROCESSED BY CRIME SCENE SUPPORT SERVICES.