Babu Owino, dhamana yake yapunguzwa kutoka milion 10 hadi 5

Ni afueni kwa mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino baada ya mahakama kupunguza dhamana yake kutoka shilingi milioni 10 hadi shilingi milioni tano.

Mbunge huyo ambaye anakabiliwa na kesi ya kujaribu kumuua DJ Evolve aliachiliwa na mahakama kwa dhamana ya shilingi milioni 10, pesa ambazo alitakiwa kulipa kwa awamu.

DJ Evolve bado amelazwa akiendelea kupokea matibabu.

Kufikia sasa Babu amelipa shilingi milioni4.4 kama dhamana na kufuatia uamuzi mpya wa mahakama sasa atahitajika kuongeza shilingi laki sita kukamilisha dhamana  yake huku kesi dhidi yake ikiendelea.

Kesi hiyo itarejelewa Machi, 20, mbali na kulipa dhamana yake Babu anahitajika kumplipia DJ Evolve gharama Za hospitali kama wajibu wake kutoka na uamuzi wa hakimu Luka Kimaru.

"Mshtakiwa ataendelea kugharamia mtibabu ya DJ Evolve kama wajibu wake wa kila siku.

Akiamua kuwa hatalipa bill hiyo ni juu yake na Mungu wake." Kimaru Alinena.