Babu Owino mwenyewe ndiye alimpeleka Dj Evolve hospitalini - Cliff Ombeta

cliff.ombeta.babu.owino
cliff.ombeta.babu.owino
Babu Owino mwenyewe ndiye aliyechukua hatua za kumpeleka DJ Evolve hospitalini baada ya kumpiga risasi shingoni, asema wakili wake Cliff Ombeta.

Isitoshe, wakili huyo alifichua kuwa Owino ndiye aliyelipa bili ya hospitali na kuapa kuendelea kulipa zaidi.

“It is Babu who took the victim to hospital and the latest is that the DJ is stable. He even paid for the medical bill and has vowed to continue paying,”Ombeta alisema.

Tazama gari inayosemekana kutumiwa na Babu Owino kumkimbiza DJ Evolve hospitalini.

Ombeta akizungumza na wanahabari alisema kuwa kuna mtu ambaye alidhani ni rafiki yake alimkaribia mteja wake kwa njia isiyo nzuri na hapo pakazuka vita.

Wakili huyo alithibitisha kuwa bastola yake Babu Owino iko mikononi mwa polisi na Babu Owino ni mmiliki halali wa bastola hiyo na ana leseni yake.

Ombeta alithibitisha kuwa hakukuwa na kesi yoyote ya mauji kwani mwathiriwa yuko hospitalini sasa hivi.

Hadi sasa hivi, Babu bado hajarekodi kauli yake kwa polisi huku uchunguzi ukiendelea.

Ombeta amewasihi wafuasi wake Owino kuwa watulivu na kutoandamana.