BAD MANNERS:Watalii sita waamatwa kwa kwenda haja kubwa kwenye hekalu moja la Peru.

machu pichu
machu pichu
Watalii sita  akiwemo mwanamke mmoja wa ufaransa  wamekamatwa huko Peru kwa kwenda haja kubwa katika  hekalu  moja linaloitumiwa kama makazi ya utamaduni wa taifa hilo  ya Machu Picchu." watalii hao sita wamezuiliwa  na wanachunguzwa na maamlaka husika kwa uhalifu huo dhdi ya makazi ya kiutamaduni’ afisa mmoja wa utawala amenukuliwa akisema siku ya jumatatu .

Watalii hao walikamatwa siku ya jumapili  baada ya maafisa wa mbuga  na polisi kuwapata katika eneo ambalo hawakufaa kuwepo  kwenye hekalu hilo kwa jina  ‘Temple of the Sun’. Wanakabiliwa na  adhabu ya hadi miaka mine jela  endapo watapatikana na hatia  kwa kutilia doa  urithi na utamduni wa Peru .

Eneo hilo la makavazi  liligunduliwa mwaka wa 1911 na  raia wa Marekani  Hiram Bingham. UNESCO  ililitaja kama eneo maalum la utamaduni linalofaa kulindwa mwaka wa 1983 .