Tanasha kwa upande wake alidhibitisha kuwa hana mipango yoyote ya kulipwa Fidia ya aina yoyote na Diamond.
Hii ni kinyume na habari zilizoenea kuwa baada ya kutengana kwao, Donna alimshtaki Diamond akidai kuwa staa huyo alimpotezea muda wa miaka miwili.
Iwapo hili ni ukweli, Tanasha atakuwa akifuata nyayo za staa wa Marekani Mariah Carey aliyemshtaki mpenziwe kwa kumpotezea wakati na akapewa Fidia ya milioni 50.
Tangia kutengana kwao, Tanasha amekuwa akijaza miotandao yake na jumbe za kujipa moyo na amekuwa akishambuliwa na mashabiki wakimrai kusahau yaliyopita na kuganga yajayo.
Hata hivyo, habari hizo kuwa anapania kumshtaki Diamond ni kama zilimfikia na alitumia mtandao wake kukana madai hayo akisema;
“Too much FAKE NEWS
out here! Let me make it
clear that there is NO
court case or whatever it
is thats being said out
there!
Can a giri live her Iife in
peace? Can we just focus
on the right & positive
things? Tha fuuuuu♀️”