Bado Zari anapendwa! Mama Dangote afichua kuwa wanazungumza na Princess Tiffah mara tatu kwa siku

Familia yake Diamond bado inampenda baby mama wake Zari Hassan licha ya hao wawili kutengana na kuachana wakiwa wamebarikiwa na watoto wawili.

Mama yake Diamond Sandra kwa muda na mara kadhaa amekuwa akimsifu kuwa mke bora kwa mwanawe kwa maana alimpa wajukuu wa kwanza.

"ZARI NAMHESHIMU. NI MWANAMKE AMBAYE NDIYE WA KWANZA KABISA KUMFANYA MWANAGU AITWE BABA. NITAENDELEA KUMHESHIMU NA KUMPA HESHIMU KWA KILE ANASCHOSTAHILI. SIMKATAZI DIAMOND PLATNUMZ KUOA LAKINI SIO HAMISA. NATAKA MWANAMKE AMBAYE ANAJIHESHIMU, MWENYE HESHIMA NA ANAYEJUA KUPIKA LAKINI SIO MOBETTO." Alisema Sandra.

Baba wa kambo wa Diamond Rally Jones aliposti video wakiongea na Princess Tiffah na kusema baadaye. Mmoja wa mashabiki wake kuona video hiyo mmoja wao aliandika,

“Hahahahhaa mama dangotee presha itanzaa kuwa juuu 😂”

Mama Dangotte hakusita bali alimjibu,

"@DR_SANDRA_MAMADANGOTE LAZIMA QUEEN KASHANZA MAWASILIANO NA MUME WANGU TENA KWA SIKU MARA 3 @PRINCESS_TIFFAH NIACHE BWANA 🤣🤣🤣." Alijibu Sandra.

Muda wa miaka miwiwli sasa Diamond hajakuwa akiwaona wanawe, hivi majuzi aliweza kuwapigia simu na video, hii ni baada ya zari kuposti ujumbe huu kwenye mtandao wake wa kijamii.

"BUT YOU DON’T KNOW WHAT YOUR KIDS EAT, OR HOW THEY SLEEP IF FEES AND MEDICAL INSURANCE IS PAID. YOU WILL NEVER PLEASE THE WORLD WHEN YOUR OWN ARE NOT HAPPY AND TAKEN CARE OF. YOU SELLING A LIE. SOME PEOPLE HAVE BECOME CLOWNS TO SOME OF US." Aliandika Zari.