Bahati aeleza kwa nini alimtumia rafiki ya mkewe kama video vixen

Mkurugenzi ama ukipenda bosi wa lebo ya EMB Kevin Bahati ameeleza kinagaubaga kwa nini alimtumia rafikiye mkewe anayefahamika kama Phoina kama video vixen kwenye kibao chake kipya cha 'Wanani'.

Akiwa kwenye mahojiano alisema kuwa aliamua kumtumia Phoina kwenye wimbo wake kwa maana ametumia mke wake kwenye nyimbo zake mbili.

Bahati alisema kuwa wimbo mmoja ambao Diana amurua aliutoa miaka michache iliyopita wa 'mpenzi' na ule mwingine ambao Diana atakuwa video vixen atautoa mwaka wa 2021.

Alizidi na mazungumzo na kusema kuwa kama msanii anapaswa kuwa na mitindo tofauti na kufanya kile atakacho wala si kile watu wengine wanahitaji.

“Sikumtumia Diana sababu yupo kwa nyimbo zangu nyingi, nimefanya naye mapenzi na kuna video yangu special inatoka 2021 bado ni yeye yupo. Isitoshe, ndio maana naitwa gospel artiste, nafaa kuwa artistic nisifanye vitu ambavyo watu wanategemea." Bahati Alisema.

Akiwa kwenye mahojiano aliisema kuwa amemaliza mwaka kama hajahojiwa na kuwa mahojiano hayo ndio ya kwanza baada ya mwaka huo mmoja kukamilika.

"Sijakuwa na sit down for over a year. Mwisho nilikaa na wewe na Mwakideu niliona mnaleta ufala saa zingine."

Bahati pia aliwahakikishia mashabiki wake kuwa ni msanii wa nyimbo za injili na wala hajabanduka.