Bahati ajibu madai kuwa rekodi ya EMB kuna mgombano na imeanguka

Ni mvurugano na mgombano ambao umekuwa katika kampuni ya rekodi ya EMB ambayo imesimamiwa na msanii wa nyimbo za injili Kevin Kioko almaarufu  Bahati.

Aliweza kujibu madai kuwa rekodi ya EMB ina mvurugu na mgombano kati ya wasanii hao na kusema rekodi hiyo ni zaidi ya huduma.

Bahati aliweza kupigwa na mpigo mkubwa wakati msanii Mr Seed aliweza kutangaza kirasmi kuwa ameweza kutoka katika rekodi hiyo ya EMB.

Akiongea Mzazi Willy M Tuva, alisema kuwa EMB ni huduma ya kukuza wasanii na wala si huduma ya kutafuta pesa.

"Rekodi ya EMB ni huduma ambayo inataka kuwainua wasanii, ni zaidi ya huduma kwa maana haitafuti ama haichukui pesa kutoka kwa msanii yeyote,

"Kwa hivyo kama haipati pesa kutoka kwa wasani basi huwezi anguka na mtu yeyote, bado tunakuwa na kujenga na ni wakati wa msanii mwingine kuingia," Bahati alielezea.

Bahati aliweza kufichua kuwa msanii Weezdom hakuwa miongoni mwa wasanii wa  rekodi ya EMB na hakuwa na mkataba wowote katika rekodi hiyo.

"Weezdom hakuwa na mkataba wowote bali ni rafiki na mimi nina roho ya baba,"Alizungumza Bahati.

Licha ya mgombano na vita vya kindani vinavyoendelea katika rekodi ya EMB, Bahati alisema kuwa ana ujasiri kuwa alifanya kazi nzuri kwa kuwainua wasanii wa kesho.

"Nina weza sema hivi kwa ujasiri, kuwa mungu amenipa neema ya kuinua watu wengine, ukitaka kumsaidia msanii lazima uweze kuweka pesa zako hapo,

"Pia kama unataka filamu bora pia inahitaji pesa, wakati huo msanii huyo ana taka kuanza huwezi pata pesa kupitia kwake, bali unapaswa uwe na moyo mzuri ili msanii huyo aweze kufanikiwa kwa kazi yake," Alisema Bahati.

Siku kadhaa zimepita rafiki ya Bahati aliweza kusema wananchi waungane ili waweze kumchangia Bahati ili aweze kulipa madeni ya wasanii ambao wako chini yake.