Bahati alinizuia kuandaa onyesho-Masterpiece afichuwa

Msanii Masterpiece amefichuWa kwanini alimuita msanii Bahati 'ibilisi' 'roho chafu kama duster' ni kwa sababu Bahati alimzuia ketekeleza onyesho awali.

Akiongea katika mahojiano alieleza kwa nini hawana uraFiki na Bahati.

"Bahati alikuwa mtu wangu, lakini kwa sasa sisi marafiki, kuna mambo ambayo yalitendeka,aliniita katika onyesho mwaka 2018 tukivuka mwaka, nilikuwa na onyesho tatu wakati huo Makueni,Thika na Nairobi." Alieleza Masterpiece.

Alifafanua zaidi na kusema

"Baada ya onyesho yangu Makueni nilitoka haraka kuelekea Thika, nilienda kwa mwendo wa kasi nilihatarisha mambo mengi,ambapo tulipofika humo

Walinzi wa Bahati walituambia waliambiwa wauambie onyesho letu limefutiliwa mbali, si kutarajia hayo kutoka kwake." Alizungumza.

Masterpiece hakutia kikomo aliendelea na kusema,

"Si kutarajia jambo kama hilo kutoka kwake,uskku huo huo alikuwa na vurugu na msanii Mr Seed kwa hivo niliondoka mahali hapo na kuenda katika onyesho lingine Nairobi."Alisema MasterPiece.

Alipokuwa akizungumza alisoma kifungu cha biblia katika kitabu cha matayo 5:8

Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu. sijaongea kwa sababu ya chuki bali na sema ukweli. nilikuwa nampatanisha na marafiki zangu ili wamsaidie katika mavazi ya onyesho." Masterpiece Alieleza.

Mwana muziki Bahati amekuwa katika vuta nikuvute na wasanii wengi  humu nchini, huku vuta ni kuvute yake ya awali ilikIwa kati yake na msanii chipukizi Peter Blessings.

Ili lazimu kamati ya wasanii kuweka mkutano ili wamuonye Bahati kwa ajili ya msanii huyo.