maxresdefault

Bahati amfokea Diana kwa ukali, alalamika kuwa Diana hawajibiki

Staa na Fundi wa muziki Bahati jana Jumamosi ameonyesha ghadhabu kubwa baada ya kufika nyumbani na kumpata kijakazi wake.

Kilichomkasirisha ni kuwa Diana mkewe alikuwa yuko hali ya kushikana akimnyonyesha mtoto wao mchanga hivi ikawa ngumu kumpakulia chakula.

Soma hadithi nyingine;

Ruto aonyesha dalili za wasiwasi, amtaja Raila Odinga Embu

Tukio hili lilifanyika katika kipindi cha Bahati Reality show kinachoonyesha maisha halisi ya staa huyu kinachoruka katika runinga hapa nchini.

Kupitia kipindi hiki, ni ishara tosha kuwa Bahati ni kati ya wanaume wasiopenda kupakuliwa chakula na vijakazi nyumbani.

Baba huyu wa watoto 3 baadae alipakuliwa chakula kama kimechelewa na akakionja tu na kuenda kulala.

Soma hadithi nyingine;

Harmonize ataja mastaa Tanzania waliojunga na Konde Gang, aitaja WCB

 “Kwa nini Irene anani-serve chakula ukiwa hapa. Ni wewe nimeoa ama ni Irene. Mbona anipakulie chakula wakati uko hapa tu. Nilioa yeye au wewe.” Bahati alimfokea mkewe walipokutana katika chumba cha kulala.

Baada ya hapo wakaanza kufokeana kwa ukali.

Diana alikasirika kuwa Bahati haoni kuwa anamshughulikia mtoto.

Gusa hapa usome hadithi za Abraham Kivuva

 

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments