Yvette Obura aliyezaa mtoto na mwanamuziki wa gospel Bahati ameanza kumtetea msanii huyo baada ya wawili hao kuwa katika pande zinazokinzana kwa muda mrefu . Obura amepuuza madai kwamba Bahati huwa hatoi hela za kumtunza bintoye .
katika hafla ya kujibu maswali katika instragram Yvette amebainisha wazi kwamba hana tatizo kuhusu juhudi za Bahati kumtunza mwanawe . Shabiki mmoja alikuwa ameashiriia kwamba mwimbaji huyo hakuwa akitekeleza majukumu yake kama baba .
Mambo hayajakuwa rahisi kati ya Bahati na Yvette baada ya msanii huyo kushtumiwa kwa kutelekeza majukumu yake kama baba na kilichofuata ni majibizano kati yao lakini baadaye waliafikiana na kukubali kufanya uzazi wa pamoja kwa binti yao .
Yvette kwa wakati mmoja alifunguka na kufichua jinsi alivyolazimika kulala njaa kwa siku kadhaa alipojifungua bila kupata usaidizi kutoka kwa Bahati lakini sasa bifu hiyo imezikwa na wanaheshimiana .