Bamba sports kupeperusha mechi dhidi ya Bournemouth na Liverpool

liverpool (1)
liverpool (1)
Jumamosi hii tarehe 7, Disemba 2019 runinga ya Bamba Sports itapeperusha moja kwa moja mechi dhidi ya Bournemouth na Liverpool. Mechi hii ambayo itasakatwa ugani Vitality, itapeperushwa mida ya saa kumi na mbili.

Vijana wa Eddie Howe wameshikilia nafasi ya 14 katika ligi kuu ya Uingereza na watakuwa na kibarua kigumu wakijaribu kuwasimamisha Liverpool, ambao wanaongoza jedwali baada ya mechi 15.

Siku chache zilizopita Liverpool walifungua mwanya wao na Manchester City hadi alama 11 na bado wako alama 8 mbele ya Leicester City ambao wako nafasi ya pili.

Hii ni kufuatia ushindi wao wa 5-2 dhidi ya Everton ugani Anfiel na kuandikisha historia baada ya kukamilisha mechi 32 vila kupoteza mechi yeyote.

Kwa upande wao, Bournemouth wamepoteza mechi zao nne baada ya kunyuka man united 1-0 mwanzoni mwa Novemba.

Zifuatazo ni mechi zingine za kutazamiwa sana wikendi hii.

Everton vs Chelsea (3:30pm)

Manchester City vs Manchester United (8:30PM)

Tottenham vs Burnley (6pm)

West ham vs Arsenal, Jumatatu (11:00)