Bandari kungang'ana kufa kupona leo dhidi ya Azam

main3
main3
Bandari FC itashuka dimbani hii leo saa kumi jioni kukipiga dhidi ya Azam ya Tanzania. Kocha wa Bandari Bernad Mwalala amesisitiza kuwa hawatakata tamaa kabla ya kipenga cha mwisho kwenye mechi hio.

Azam ndio mabingwa watetezi wa taji hilo na wamo katika nafasi ya pili kwenye kundi B wakiwa na alama 3 huku bandari wakishikilia nafasi ya tatu na alama mbili.

Ushindi wa aina yoyote utawapeleka Bandari katka atua ya robo Fainali. KCCA wanaongoza kundi hilo kwa alama nne baada ya kucharaza Azam na kutoka sare na Bandari huku.

"Wao ndio mabingwa watetezi wa taji hili na hivyo wakatakuwa wanang'agania kwa udi na uvumba kuingia ndani ya Nane bora. Hata hivyo, tunawahakikishia kuwa hatukati tamaa hadi dakika ya mwisho kipenga kikipulizwa,"Mwalala alisema.

Kwingineko Gor Mahia itashuka dimbani siku ya jumapili kukabana koo na KMKM ya Zanzibar. Gor Mahia tayari imefuzu kwenye hatua ya robo fainali ya kombe la CECAFA.