Bando zinayeyuka Insta, Mwonekano wa Stivo Simple Boy unakosha wengi (+Picha)

48762FF2_B5AF_447D_A41C_387A7BC0112F__1569246456_85526
48762FF2_B5AF_447D_A41C_387A7BC0112F__1569246456_85526
Picha za mwanamuziki kutoka mtaa wa mabanda wa Kibra zinayeyusha bando za watu Insta .

Kijana huyu sasa ndio gumzo kitaani baada ya kuvuma na bonge la ngoma.

Stivo Simple Boy aliteka vichwa vya habari alipovamia tansia ya muziki na mkwaju wa Mihadarati.

Ngoma hii ilipokelewa vizuri katika mitandao ya YouTube huku wengi wakionyesha kuipa shavu talanta yake.

Soma hadithi nyingine;

Kwa sasa Stivo amekuwa gumzo Insta na suti za bluu;

https://www.instagram.com/p/B2wCfkVF9Ok/

Mastaa nchini akiwemo Chipukeezy, Khaligraph Jones walionyesha nguvu kubwa ya kuinua talanta ya Simple Boy.

Stivo alikuwa anafanya kazi ya mjengo kabla avume zaidi katika mitandao ya kijamii.

Rapa Khaligraph aliwahi kufoka jinsi vyombo vya habari vilikuwa vinamshobokea kijana huyu katika mahojiano.

Soma hadithi nyingine;

Kulingana na Khaligraph, baadhi ya vyombo vya habari vingemtumia kupata hadhira na baadaye kumtema.

“Kila mtu sasa anataka kuoenekana na huyu kijana...kumuita katika interviews ili kuzidisha pato badala ya kuongea naye kuhusu muziki." Khaligraph

Khaligraph alikuwa wa kwanza kumuomba Chipukeezy kuhakikisha kuwa Stivo yuko sawa.

Chipukeezy alimjibu kuwa,

"Stivo ni msanii wa kawaida, kwa hivyo akiitwa katika interview anapaswa kufika ili auze muziki wake."

"Nimefanya nilichopaswa kufanya na sasa Simple Boy ni balozi wa Nacada..." Alisema chipukeezy.

Kwa sasa Stivo Simple Boy anatesa zaidi katika mitandao Insta.