Baraza la magavana lataka hazina ya kitaifa itoe mgao wa fedha za kaunti

baraza la magavana
baraza la magavana
Baraza la magavana nchini limefika mahakama ya juu likiitaka kuiamuru hazina ya kitaifa kutoa mgao wa fedha za kaunti wa mwezi wa Novemba na Disemba kwani kucheleweshwa kunakoshuhudiwa kunaathiri utendakazi wa kaunti.

Haya ni kulingana na mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya aliyesema ni kinyume cha katiba kusimamisha mgao wa kaunti bila ya mchakato wa kisheria uliotiwa sahihi na bunge la kitaifa au lile la seneti.

Amesema mgao huo wa fedha wa jumla ya shilingi bilioni 316 unapaswa kutolewa kwa serikali za kaunti ifikapo tarehe 15 ya kila mwezi.

Aidha ameilaumu hazina ya kitaifa kwa kufeli kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa serikali za kaunti zinapokea mgao wao wa fedha kwa wakati ufaao akisema hili limeathiri sana majukumu ya seriakali hizo.

-CALISTUS LUCHETU