Baraza la walemavu waomba usaidizi kupunguza visa vya ujanisi

wheelchair001
wheelchair001
Baraza la walemavu nchini limeitaka idara ya usalama kuwachukulia hatua za kisheria washukiwa wa unajisis wa watu walio na ulemavu kama njia moja ya kukabiliana na ongezeko la visa vya unajisi wa watoto walemavu hasa eneo la mkoa magharibi.

Mwenyekiti wa baraza la walemavu nchini dakta david sangok amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza visa hivyo ambavyo vimeongezeka hasa katika eneo la magharibi.

Mweneykiti huyo aliyasema haya katika shule ya watoto walio na ulemavu na lwanya ambapo alidokeza kuwa wameanzisha mradi wa kujenga mabweni ya wasichana wenye upungufu wa kimaumbile ili kuepukana na tishio la kunajisiwa.