Barcelona wamewasilisha ofa ya pauni milioni 90 ili kumsajili Neymar

Barcelona wamewasilisha ofa ya pauni milioni 90 kwa kiungo wa PSG Neymar.

Klabu hiyo ya La Liga imeipa PSG orodha ya wachezaji 6 ambao huenda wakajumuishwa kwenye mkataba huo, wakiwemo Philippe Coutinho, Ousmane Dembele, Ivan Rakitic, Nelson Semedo, na Malcom. Mchezaji wa sita bado hajulikani ni nani.

Inaaminika kwamba klabu hiyo ya Ufaransa inataka zaidi ya pauni milioni 200 kwa mchezaji huyo wa miaka 27. PSG ilimsajili Neymar kwa kitita cha pauni million 200 kutoka Barcelona mwaka wa 2017.

Arsenal inajaribu kuwasajili wachezaji maarufu walio ghali zaidi msimu huu kulingana na mkufunzi Unai Emery. Baadhi ya makundi ya mashabiki na wanablogu wametaka kuwepo kwa mabadiliko katika klabu hiyo na Emery amesema kuwa The Gunners inatafuta wachezaji wenye tajriba ya juu katika uhamisho wao.

Tayari maombi yao ya kutaka kumnunua winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha na beki wa kushoto wa Celtic Kieran Tierney yamekataliwa.

Wilfried Zaha ameiambia Crystal Palace kwamba anataka kuondoka klabu hiyo huku ikiwa Arsenal wanataka kumsajili. Kiungo huyo wa umri wa miaka 26 alisema haya baada ya kuregea Palace kutoka kuichezea Ivory Coast katika kipute cha AFCON.

Palace tayari wamekataa ofa ya Arsenal ya pauni milioni 40 lakini Gunners wanatarajiwa kuongeza kitita hicho hivi karibuni. Zaha hana matatizo yoyote ya kibinafsi na kocha Roy Hodgson au Palace, lakini anataka kujidhihirisha kwa mojawapo ya vilabu vikubwa zaidi vya Uropa.