'Beach Boys' wanawakera watalii huko Pwani

Imebainika sasa kwamba Kenya hupoteza asilimia 90 ya watalii wanaotembelea eneo la pwani kutokana na usumbufu unaosababishwa na vijana wajulikanao kama 'beach boys'.

Mwenyekiti wa kamati ya kilimo na uvuvi Adan Haji amesema ili kuimarisha sekta ya utalii, suluhisho linahitajika la kuwaondoa vijana hao kutoka kwa fukwe za bahari na kupelekea kuboreka kwa sekta hio kwa asilimia 25.

Anasema suluhu hilo linatakiwa kuwa kuanzishwa kwa njia za kutumika na wanunuzi bidhaa katika barabara zinazoelekea ufuoni, ambazo zitahakikisha kua biashara zipo kwenye barabara hizo na kuwawacha watalii wa kigeni kufurahia wakiwa likizoni.