Beef yangu na yeye ni ya biashara tu! Harmonize afunguka kuhuisiana na uhusiano wake na Diamond

harmonize-tattoo-cover
harmonize-tattoo-cover
NA NICKSON TOSI

Wakati mwingine kuingiza undugu kwenye biashara huwa na changamoto zake za kila mara. Harmonize na Diamond walikuwa marafiki wa karibu sana kutokana na ufanisi wa miziki mbalimbali ambayo walikuwa wanaifanya pamoja.

Hatua ya Harmonize ya kutoka kwenye lebo ya WCB ilionekana kuibua mzozano baina ya wasanii hao wawili, jambo lililomfanya Konde boy kulipa dau nono la hela kabla ya kutengana kabisa.

Harmonize baada ya kutoka kwenye lebo hiyo, alianzisha lebo yake kibinafsi ya Konde Music World ambapo alimsajili msanii Ibraah kutoka kwa lebo ya Alikiba.

Akiwa kwa mahojiano na shirika moja, Harmonize alielezea hivi kuhusiana na uhusiano wake na Diamond.

I respect and he is doing a good job. I do not want to lie to you, I am cool with him. We are cool bro we are from the same country, Tanzania so we cool. We used to be friends and you know that but now we are not I do not want to lie to you. Nothing bad it is just that we are not working together anymore. That is what I am trying to say but we do not have any problem with each other. Some business reasons nothing personal. Alisema Harmonize.

Wawili hao kabla ya kutengana, walikuwa wamefanya nyimbo kama  Kwangwaru, wimbo ambao uliwafungulia milango wasanii hao wote wawili.

Wakiwa marafiki wakati huo, ifahamike kuwa wakati mwingi Harmonize alikuwa anapendelea kuwakosoa wale waliokuwa wanamhukumu Diamond kabla ya uhusiano huo kutifuka.