Beki wa PSG Layvin Kurzawa atajiunga na Arsenal kwa mkataba wa miaka 5

rsz_kurzawa_
rsz_kurzawa_
Beki wa Paris St-Germain na Ufaransa Layvin Kurzawa mwenye umri wa miaka 27, atajiunga na Arsenal kwa uhamisho wa bila malipo wakati kandarasi yake itakapokamilika mwezi Juni na amekubali mkataba wa miaka mitano na The Gunners. Kwingineko Arsenal itajaribu kumsajili beki wa Bayern Munich na Ujerumani Jerome Boateng wa miaka 31, kwa mkopo mwezi huu kabla ya kuwasilisha ombi la pauni milioni 50 ili kumnunua beki wa kati wa Ufaransa Dayot Upamecano mwisho wa msimu.

Inter Milan wako tayari kulipa kitita cha pauni milioni 11 na marupurupu mawili ili kumsajili Christian Eriksen kutoka Tottenham mwezi huu.

Inter awali ilikua imetoa pauni imilioni 8.5 kwa ajili ya Eriksen lakini wakaambiwa kuwa Spurs wanamwekea thamani maradufu ya hiyo. Ajenti wa kiungo huyo wa kati raia wa Denmark Martin Schoots atakutana na mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy hii leo kujadili hali hio.

Frank Lampard anasema yuko tayari kuwasajili wachezaji kwa mikataba ya muda mfupi mwezi huu na hajafutilia uhamisho wa mshambulizi wa PSG Edinson Cavani. Kandarasi ya raia huyo wa Uruguay mwenye umri wa miaka 32 inakamilika mwishoni mwa msimu huu lakini amewaambia mabingwa hao wa Ufaransa kwamba anataka kuondoka mwezi huu baada ya kuanza mechi nne tu katika Ligue 1. Lampard amesema wazi kua anataka kumsajili kiungo mpya mwezi huu.

Aston Villa wamekamilisha mktaba wa pauni milioni 10 kumsajili mshambulizi wa Genk Mbwana Samatta. Raia huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 27 ametia saini mkataba wa miaka minne na nusu utakaolingana na kupewa kwake kibali cha kufanya kazi. Amefungia Genk mabao 10 katika mashindano yote msimu huu ikiwemo bao ugani Anfield dhidi ya Liverpool, katika ligi ya Mabingwa. Atakuwa mtanzania wa kwanza kucheza katika ligi ya Primia.

Real Madrid wamekamilisha usajili wa kiungo wa kati raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 18 Reinier Jesus kwa kitita cha pauni milioni 26. Reinier, ambaye ametia saini mkataba wa miaka 6 na miamba hao wa Uhispania alichezea Flamengo kwa mara ya kwanza kwenye timu kubwa, Julai mwaka uliopita. Alikua kwenye kikosi kilichoshinda ligi ya Brazil na Copa Libertadores msimu uliopita. Alikua mfungaji mabao bora zaidi kwenye kipute cha kombe la dunia kwa wachezaji wa chini ya miaka 16 huko Dubai mwaka 2018.

Kocha mkuu wa Malkia Strikers Paul Bitok anavitaka vilabu vya voliboli humu nchini kujiyahidi kuwa na utaalamu kama vilabu vya Kaskazini mwa Afrika. Bitok ambaye pia ni kocha wa timu ya kinadada ya KCB aliwaambia kinadada hao kufuata ushauri wa rais wa kuufanya mchezo huo kuwa tajriba yao na kutumia vizuri talanta yao.

Aliwasaidi Malkia kujikatia tikiti ya pekee barani Afrika katika michezo ya Olimpiki jijini Tokyo mapema mwezi huu na anasema ni lazima wajitahidi kufikia viwango vya kimataifa.