Betty Bayo aeleza mahangaiko YouTube, sifa za Victor Kanyari kwake

kanyari__1571897095_82588
kanyari__1571897095_82588
Aliyekuwa mke wa muhubiri tata Victor Kanyari, Betty Bayo amefunguka kuhusu vita anazozipiga dhidi ya mahangaiko na masimango maishani mwake.

Akisimulia katika mtandao wake wa YouTube, Betty anaeleza jinsi alivyotokea katika hafla yake ya harusi katuika hali ya kufedhehesha.

"Mtu anaweza kujiuliza iwapo nishai zama katika lindi la mawazo, ndio nishawahi..."

"Nilipigika zaidi nilipojipata nimevaa kandambili katika hafla yangu ya harusi..."

"Sikuwa nimechana nywele wala kujipaka mafuta yoyote..." Alifunguka mama huyu.

"Akilini mwangu nilitoka nyumbani kama nina nia njema ya kufanya harusi ila mipango ya kutokea kama nimechakaa haikuwepo..."

Katika mahojiano ya awali, Kanyari alisema kuwa yeye na Bayo walikuwa wanawalea na kuwasetiri watoto vyema.

Kauli ya muhubiri huyu ililenga tetesi kuwa kuna uwezekano kuwa ametelekeza watoto.

"Ninapopata wakati huwa tunakaa na watoto na kuzungumza mengi kuhusu maisha yao na nisipopata muda huo huwa naongea na Mungu..."

"Huwa namwambia Mungu awalinde..."

"Betty hajawahi kuninyima ruksa ya kuwaona watoto. Nikataka kuenda kuwaona sasa naenda tu. Ni mke na mama mzuri..." Alisema Kanyari

Wawili hawa walioana mwaka wa 2012 katika hafla ya faragha na ndoa yao kuvurugika baada ya miaka 3.