Betty Kyalo afunguka kuhusu masaibu ya ugonjwa wa mtoto wake Ivanna

Screenshot_from_2019_12_31_09_35_17__1577774144_59814
Screenshot_from_2019_12_31_09_35_17__1577774144_59814
Mtangazaji wa kituo cha K24 Betty Kyalo amefunguka kuhusu hali ya ugonjwa iliomtatiza bintiye kwa muda mrefu.

Mtoto wake Ivanna alipatwa na hali ya kupoteza fahamu na hivyo kumbidi alazwe katika chumba na ambacho afya yake ingeangaziwa kwa kina.

https://www.instagram.com/p/B6iyNP3lF-I/

Madaktari katika hospitali kuu ya Nairobi walizamia swala nzima ili kubaini kilichosababisha hali hii.

“Kadri ya uchunguzi uliofanywa na daktari, hakuna dalili zozote za ugonjwa kuonekana. Tulifanyia sehemu zote za mwili wake tukaambulia patupu," aliandika Betty Insta.

 Akisimulia kisa hiki, Betty amedokeza kuwa mwanawe hangeweza kula wala kutembea

“Mwaka huu ukianza, mtoto wangu Ivanna alipatikana na maradhi isiyokuwa ya kawaida...." Alisema Betty.

https://www.instagram.com/p/B6sXPcPlG7a/

Betty anaelezea jinsi alivyozongwa na fikra kwa kipindi kirefu.