Biashara ya ngono! Makahaba Vihiga wataka kuruhusiwa kuuza visima usiku

NA REHEMA OSANYA

Wachuuzi wa ngono katika kaunti ya Vihiga sasa wanautaka usimamizi wa kaunti hiyo kuwapa misaada ili kujikimu wakati huu mgumu wa kiuchumi kufuatia marufuku ya kutotoka nje nyakati za usiku.

Makahaba hao ambao kwa sasa hawawezi kuuzia wanaume vitumbua vya nyama mbichi wanadai kukabiliwa na changamoto za kifedha kutokana na janga la Corona. Warembo hao ambao biashara yao hunoga gizani kwa sasa wamefungiwa kitega uchumi chao kutokana na masharti ya kutotoka nje usiku.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao kaunti ya Vihiga Janet Minayo almaarufu ‘Take Away’na katibu wake Kitagwa Ondisa, walisema kuwa tangu kuzuka kwa janga la covid 19 hali ya biashara yao imekumbwa na ukosefu mkubwa wa wateja ambao hurudi nyumbani mapema.

Mama Take Away ametoa wito kwa kaunti hiyo kuzingatia changamoto zao msimu huu, ikiwemo kuwataka maafisa wa usalama eneo hilo kuwaruhusu kuendesha biashara zao ili kujikimu na mahitaji yao.