Biashara ya Vera imemfanya kujenga kasri Mombasa

Maajuzi Vera Sidika alilazimika kusafiri hadi kaunti ya Mombasa ili kutathmini namna shughuli ya ujenzi wa nyumba yake ulikuwa unaendelea.

Sidika aliwashangaza wengi baada ya kutundika picha mitandaoni zikionyesha namna ujenzi wa kasri lake ulivyokuwa unaendelea.

 ‘CAN’T WAIT TO WORK ON THIS PLACE. SO MUCH WORK TO BE DONE BUT THE OUTCOME WILL BE MIND-BLOWING. COMING SOON’, aliandika Vera

Siku chache zilizopita, taarifa zilichipuka kuwa mwanasosholaiti huyo alikuwa hana pesa baada ya kutofautiana na mpenzi wake japo akatupilia mbali madai hayo.

Amefichua kuwa alianza kuishi kwa nyumba ambayo alikuwa analipa shilingi 3,500 kila mwezi.

‘LIFE IS INDEED A JOURNEY, YOU NEVER WAKE UP & HAVE IT ALL PERFECT! YOU NEED TO FEEL THE STRUGGLE & PAIN & BE PATIENT BEFORE SEEING BETTER DAYS. I REMEMBER WHEN I CAME TO NAIROBI I USED TO LIVE IN A BEDSITTER IN KAHAWA WENDANI KSH. 3,500 MONTHLY. IT WAS THE LIVING ROOM, DINING, BEDROOM, KITCHEN, BATHROOM ALL IN ONE SQUEEZED SPACE…AND TODAY KSH. 3,500 IS WHAT I’D USE ON-CALL CREDIT DAILY. SEE HOW GOD WORKS! PRAYER; MAJOR KEY,’aliandika Vera