Bibi yangu alinitenga alipogundua kuwa nilikuwa na mpenzi mwingine

Willie alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Millie akidai kuwa amejaribu kumuomba msamaha lakini amenyamaza tu.

"Wakati nilikuwa namuoa nilikuwa na mpenzi mwingine na ilikuwa tu urafiki, ambaye Millie alikuja akamjua.

Nilimueleza na akakubali na baadaye huyo mpenzi wangu akaja nyumbani ku hakikisha kuwa nimeoa na alipopata Millie tukaanza mzozano.

Baada ya Lucy kuondoka akampigia simu Millie baada ya miezi kadhaa na hapo Millie alianza kunishuku kuwa mie ndiye niliyempea nambari yake na baada ya siku kadhaa nilipata Mke wangu akiwa amefunganya virago na kuondoka." Alijieleza Willie mwenye umri wa miaka 27.

Millie alizima simu baada ya kuskia sauti ya watangazaji Gidi na Ghost.

Isitoshe wawili hao walikuwa pamoja kwa miezi miwili pekee.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be