Bifu yaibuka baina ya Harmonize na Diamond kuhusu ni yupi mkali kati yao

NA NICKSON TOSI

Harmonize amekua akifanya bidii zaidi tangu aondoke lebo ya WCB inayoongozwa na Diamond, na sasa wasanii hao wameonekana kama watu ambao hawapatani siku hizi  licha ya Diamond kusifia hatua ya Harmonize ya kutoa albamu ya nyimbo 18.

Kama mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize alimshukuru Mola kwa kumwezesha kuwa na kampuni yake kibinafsi na hata mafanikio ambayo ameyafikia tangu aanze muziki.

Hata hivyo hatua ya Harmonize ya kufunganya virago na kutoka lebo ya WCB, ilichukuliwa kama hatua ya kujiendeleza kimuziki japo uamuzi huo wake ulimfanya kupoteza marafiki katika lebo ya WCB.

Siku chache tu baada ya Diamond kuonyesha kwenye mitandao ya kijamii kasri lake ambalo anaishi kwa sasa, Harmonize hakusalia nyuma kwani alitundika picha ya msanii ambaye amemwandika chini ya Lebo yake kisha kuonyesha jumba la kifalme ambalo anaishi ndani, swala ambalo lilionekana kama njia ya kumjibu Diamond kuwa wapo wengi waliofanikiwa zaidi ya yeye.

Harmonize amemsajili msanii Ibraah ,ambaye kando na kuimba ni mwandishi wa nyimbo tena.

Baadhi ya picha alikuwa ametundika Diamond akiwa kwa makazi yake ndizo hizi hapa.

Harmonize hakusita kuonyesha wafuasi wake naye kasri ambalo anaishi ndani na baada ya kuona picha hiyo ya Diamond, alimua kufichua ukubwa wa nyumba yake.

Inadaiwa kuwa bifu baina ya wasanii hao wawili ilianza baada ya Harominze kuanza kuwasajili wasanii wapya, hali iliyomfanya Diamond kusema kuwa amemsajili Zuchu msanii chipukizi na mwanawe Hadija Kopa kwenye Lebo ya WCB.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO