Bila pesa, shule za kibinafsi sasa zaomba msaada kutoka kwa serikali

Shule za kibinafsi nchini sasa zinataka msaada ya kifedha kutoka kwa serikali ili kuziwezesha kulipa walimu mishahara wakati huu wa janga la virusi vya corona.

Shule nyingi za umma zilisitisha mishahara ya walimu wao kutokana na athari za janga la corona ambalo lilipelekea kufungwa kwa shule zote nchini. Shule hizo hata hivyo zinashikilia kwamba kamwe hazitawaachisha kazi walimu hao lakini kwa sasa hazina mbinu za kuwalipa mishahara.

Huku shule zikitarajiwa kufungwa hadi mwezi Septemba, afisa mkuu mtendaji wa muungano wa shule za kibinafsi Peter Ndoro siku ya Jumanne alisema kwamba huenda walimu katika shule hizi wakakosa kulipwa kwa takriban miezi mitano.

"Kama tu sekta ya utalii, tumeomba wizara ya elimu na hazina ya kitaifa kuzingatia maslahi ya walimu katika shule za kibinafsi ambao pia kwa sasa ni miongoni mwa watu walioathirika zaidi na janga hili ili waweze kugharamia mahitaji yao ya kimsingi ," Ndoro alisema.

Hata hivyo alidinda kuelezea undani wa mashauriano au kiasi cha pesa kinachotakikana ikiwa serikali itakubali ombi lao na kushikilia kwamba bado mazungumzo yanaendelea.

"Sekta hii imefungwa kabisa. Shule hazina namna zingine za kupata pesa isipokuwa kutokana na karo zinazolipwa,"  alimbia the Star kwa njia ya simu.

Mshahara wa mwisho walimu wengi wa shule za kibinafsi kulipwa ulikuwa wa mwezi wa Machi