Binti kiziwi azungumzia wakati alipokuwa gerezani China

Screenshot-from-2020-02-26-11_51_55
Screenshot-from-2020-02-26-11_51_55
Baada ya kumaliza miaka saba katika jela za China Sandra Khan almaarufu video vixen aliyefahamika sana katika wimbo wa binti kiziwi alizungumzia zamu yake alipokuwa katika gereza hizo.

Sandra alirudi nchini Tanzania mwishoni mwa mwaka wa 2019.

Akizungumza akiwa katika mahojiano na runinga moja nchini Tanzania Khan alisema kuwa baada ya kupewa kifungo cha miaka saba familia tu ndio walikuwa wanamjulia hali na kuzungumza naye.

Aliongeza na kusema kuwa marafiki wake wote walimtoroka na kumuacha.

Sandra ambaye ni mama wa mtoto mmoja alisema kuwa alipeza sana kuwa mama na hata kumlea mwanawe, Alipotoka jela alisema kuwa alijawa na hisia nyingi na kilio alipomuona mwanawe aliyemuacha na miaka nne lakini amempata amekua sana.

Hakusita wala kunyamaza bali aliwaomba jamaa na familia yake msamaha kwa kitendo alichokifanya.

Alipoulizwa kama atarudiana na aliyekuwa mpenzi wake Z Anto alijibu na kusema "Muda tu ndio utanena na kutuambia"

Wawili hao waliachana miaka mitatu kabla Sandra afungwe kwa ajili ya dawa za kulevya, alipokuwa gerezani Sandra alisomea shahada ya Human Resource na Psychology.

Sasa yupo nchini Tanzania na anatafuta kitu cha kufanya ili kupata riziki

“NIMEAMUA KUMUWEKA TENA BINTI KIZIWI KWENYE VIDEO YA WIMBO WANGU MPYA WA ‘NICHAPE’ KWASABABU MUDA ALIOUPOTEZA AKIWA JELA CHINA NI MWINGI, ALIFAHAMIKA KUPITIA MUZIKI NIKAONA NIMRUDISHIE HADHI YAKE NA JINA LAKE, ITAMSAIDIA KUFANYA BIASHARA ZAKE NYINGINE KAMA SALOON,” Z Anto Alinena.