Bintiye Mandela Zindzi alipatikana na virusi vya COVID 19

Zindzi Mandela,  bintiye  rais wa  zamani wa afrika Kusini Nelson  Mandela  alipatikana na virusi vya corona  katika siku ambayo aliaga dunia .

Aliaga dunia katika hospitali moja jijini  Johannesburg  mapema wiki hii akiwa na umri wa miaka 59 .

Mwanae  Zondwa  Mandela  ameliambia shirika habari la SABC  kwamba haijabainika iwapo ugonjwa huo ndio uliosababisha kifo chake . Familia hiyo inangoja ripoi ya upasuaji wa mwili wake

" kwa sababu kulikuwa  na kiimo kilichoonyesha kwamba alikuwa na COVID 19 inabidi tufuate kanuni zilizopo sasa kuhusu jinsi ya kuwazika watu wenye virusi hivyo’ amesema

Amenukuliwa akisema mamake atazikwa ijumaa asubuhi

Zindzi  alikuwa balozi wa Afrika kusini nchini  Denmark .

Alizaliwa Disemba tarehe 23 mwaka wa 1960  kwa Nelson Mandela na Winnie Mandela .

Zindzi  amewaacha watoto wanne , Zoleka, Zondwa, Bambatha  na  Zwelabo.