Bintiye Waititu Monica Njeri, kufunga ndoa siku ya kesho

unnamed (4)
unnamed (4)
Mwanake Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu, Monica Njeri, atakuwa anafunga ndoa siku ya kesho.

Monica, ni daktari anayeolewa na Dr Nyotu Gitau. Kulingana na mtandao wa kijamii, Nyotu alisomea Ubunifu wa Afya katika chuo kikuu cha Cape Town na Shahada ya Madawa na Shahada ya Upasuaji katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

Kwa upande mwingine, Njeri, ni mhitimu wa udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi. Yeye ni daktari mwandamizi katika Hospitali ya Gatundu Level 5 baada ya kuajiriwa na serikali ya Kiambu. Hapo awali, alifanya kazi katika Hospitali ya Kenyatta.

Harusi hiyo imepangwa kufanyika katika Kanisa la PCEA Evergreen huko Runda kutoka saa 10:30 mchana. Mapokezi yatafanyika kwenye Windsor Golf na Country Club na sherehe hiyo itahudhuriwa na watakaokuwa wamealikwa pekee.

Hata hivyo mke wake Ferdinand Waititu na mtoto wake Monica Njeri wanangoja kushtakiwa kwa mashtaka ya kutotii sheria na mashtaka mengine.

Soma mengi