Blog

Njama ya Ruto na TangaTanga ‘kuiteka nyara’ Jubilee kutoka kwa Uhuru Kenyatta

Wandani wa Ruto sasa wanamsukuma ‘kuteka nyara’ chama cha tawala cha Jubilee kutoka kwa uongozi wa Uhuru Kenyatta.

Haya yanajiri baada ya mkutano wa jamii za GEMA kukutana katika ikulu ndogo ya Sagana kujadili maswala ya BBI na kuziba nyufa zinazofanya wabunge kugawanyika katika vikundi vya TangaTanga na Kieleweke.

Kundi la wabunge wa TangaTanga lipo katika juhudi za kuchukua kiti alichokikalia Uhuru mwaka wa 2022.

Hawa ni wabunge kutoka bonde la ufa na mlima Kenya waliokaidi wito wa rais wa “tuache kampeni tufanye kazi kwanza.”

Ruto avunja kimya kirefu kuhusu mkutano wa Gema Sagana

 Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, wengi wa wabunge wanahoji kuwa tukio la Uhuru kuita mkutano wa mlima Kenya wala sio wabunge wote wa chama cha Jubilee ni ishara kuwa hana nia njema na maisha ya usoni ya chama hiki.

Ndoa ya Ruto na Uhuru inaonekana kusambaratika baada ya ‘Handshake’ iliyofanyika mwaka jana.

Wandani hawa wa Ruto wameapa kuyapuuzilia mbali mapendekezo ya BBI punde tu yatakapochapishwa.

Wachanganuzi wa siasa wanahoji kuwa Ruto anatakiwa ahakikishe hakuna nyufa zozote katika chama hiki iwapo atataka kutwaa ushindi na kuchukua hatamu ya urais mwaka wa 2022.

 

(+ Picha )Mke wa Mwanahabari Richard Muema aliyepigwa risasi Kasarani afunguka

Katika mkutano uliofanyika bonde la ufa Jumamosi, Ruto aliwaonya waasi wa chama cha Jubilee wanaotapatapa vyama vingine watoke au wajirudi.

Wandani hawa wa Ruto wanapendekeza uchaguzi wa chama ufanyike mwaka ujao 2020 ili kuwachuja ‘watu wa rais Uhuru’ katika nyadhifa za uongozi.

“Lengo la chama cha Jubilee kwa sasa linafaa kumzuia Raila Odinga kuvunja chama kama jinsi alivyofanyia vyama vilivyotawala. Alivunja KANU, NARC, CORD na sasa anakujia Jubilee.” Cherargei alisimulia Daily Nation.

“Ni wazi kuwa Ruto ni yeye pekee anayetaka chama hiki kiwepo na anafaa ‘akimbie’ nacho” ,Alisema Bwana Chebunet.

Je, Ruto atafanikiwa kufanya jinsi wandani wake wanamshauri?

Ruto avunja kimya kirefu kuhusu mkutano wa Gema Sagana

Hatimaye Ruto amevunja ukimya wake kuhusiana na mkutano wa Gema uliofanyika Ijumaa.

Katika mkutano huo,Uhuru aliwaonya wanaopinga BBI na kuwahimiza viongozi wa mlima Kenya kuunga mkono ‘Handshake’

Uhuru alisema tayari matunda ya BBI yalionekana katika uchaguzi mdogo wa Kibra wa Novemba 7.

(+ Picha )Mke wa Mwanahabari Richard Muema aliyepigwa risasi Kasarani afunguka

“Katika miaka yangu yote sijawahi ona kampeni ya amani Kibra. Kuna baadhi ya watu wachache walirushiwa mawe lakini hatukuona duka likichomwa au watu wakiwa na wakati mgumu wakienda nyumbani,” Uhuru alisema.

“Iwapo uchaguzi unaweza ukafanywa Kibra na watu hawatapoteza mali yao au maisha yao basi hiyo ni ushindi na watu wanafaa kujifunza kutokana na hilo.” Uhuru.

Ruto ambaye amekuwa mnyamavu kuhusiana na matukio ya kisiasa yaliyofanyika Sagana ameamua kutoa wazo lake.

Kupitia mtandao wa Twitter, Ruto amesema kuwa mkutano wa Ijumaa Sagana uliziba nyufa na kukifanya chama imara zaidi.

Ugonjwa anaougua Othuol Othuol , namba yatolewa kuchanga hela

Haya yanajiri huku chama cha ODM kikimsifia sana Rais Uhuru Kenyatta kuhusu tamko la lengo la BBI katika mkutano uliofanyika Sagana.

Aidha, mwenyekiti wa ODM amesema kuwa Uhuru anathamini sana ‘Handshake’ iliyofanyika kati ya Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.

Mengi yanasubiriwa kufanyika katika ulingo wa kisiasa tukisubiri mwaka wa 2022.

ODM yatoa kauli kuhusiana na mkutano uliofanyika Sagana IJumaa

Chama cha ODM kimemsifia sana Rais Uhuru Kenyatta kuhusu tamko lake kuhusu lengo la BBI katika mkutano uliofanyika Sagana.

Aidha, mwenyekiti wa ODM amesema kuwa Uhuru anathamini sana ‘Handshake’ iliyofanyika kati ya Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.

(+ Picha )Mke wa Mwanahabari Richard Muema aliyepigwa risasi Kasarani afunguka

Kupitia kauli iliyochapishwa leo Jumapili, ODM inaona msimamo dhabiti wa Uhuru Kenyatta katika juhudi za kuunganisha Taifa la Kenya.

Mbadi amesema kuwa alifuatilia kwa makini kilichoenedelea katika mkutano wa Sagana.

 Katika mkutano huo wa Ijumaa, Rais aliwaonya wanaopinga BBI hata kabla hawajapata nafasi ya kuiona.

Uhuru alisisitiza kuwa BBI na ‘Handshake’ zina umuhimu mkubwa wa kuleta amani Kenya na wala haipangi mipango yoyote ya siasa za 2022.

Mkutano huu wa pili wa Rais Kenyatta ulilenga kuziba nyufa zilizosababishwa na vikundi vya TangaTanga na Kieleweke.

Aidha, ODM imesema Rais alifurahishwa na uchaguzi mdogo uliofanyika Kibra Novemba 7,

Aliyetekwa nyara’ apatikana na mpenzi akijipa raha Thika Road Mall, DCI yaeleza

“Katika miaka yangu yote sijawai ona kampeni ya amani Kibra. Kuna baadhi ya watu wachache walirushiwa mawe lakini hatukuona duka likichomwa au watu wakiwa na wakati mgumu wakienda nyumbani,” Uhuru alisema.

“Iwapo uchaguzi unaweza ukafanywa Kibra na watu hawatapoteza mali yao au maisha yao basi hiyo ni ushindi na watu wanafaa kujifunza kutokana na hilo.” Uhuru.

Diamond, Tanasha wanahatarisha kufungwa jela Tanzania

Staa na nguli wa muziki Afrika Diamond Platnumz na Tanasha Donna huenda wanahatarisha kutiwa nguvuni na mamlaka nchini Tanzania katika kipengele kipya cha kuhalalisha ndoa.

Nchi jirani ya Tanzania inasukumia kuwepo na urasmi wa ndoa kati ya raia wao.

Diamond na Tanasha ni miongoni mwa wanandoa nchini humo ambao hawajaona rasmi.

View this post on Instagram

Waiting on #wasafifestival19 like…..

A post shared by Tanasha Donna Oketch (@tanashadonna) on

Mkondo tofauti wa hekaya za Paul Manyasi, DCI yatoa kauli inayokanganya zaidi

Serikali ina mtazamo kuwa mtindo wa wanandoa kuishi chumba kimoja bila kuoana rasmi ni chanzo cha watoto wanaorandaranda mitaani.

Ndoa hizi zikivunjika, watoto hupata tabu kubwa sana na wengi huishia kuombaomba kwenye vichochoro.

Andrea TSele alitangaza kuwa wanandoa kama hao wakamatwe na kutiwa nguvuni ili wajue ubora wa kufunga ndoa.

TSele alikuwa akizungumza katika kata ndogo ya Mavanga jimbo la Ludewa Njombe .

Kinachomkera TSele ni wanaume wanaowakimbia wamama baadaye ya kuwatunga ujauzito.

” Na hawa watu wanastahili watiwe mbaroni kwa kuwa hawataki kuhalalisha ndoa ilihali wanataka kuishi kama mume na mke…” Tsele.
Tsele alihofia sana uongezeko wa watoto wanaorandaranda mitaani.
Zari The Boss Lady amenukuliwa kusema kuwa Diamond hatoi usaidizi unaotakiwa kwa watoto wao.
Hapo awali, Zari alimuonya Tanasha kuwa ajitayarishe kulea mtoto peke yake.
Inadaiwa kuwa Tanasha na Diamond wanaishi katika chumba kimoja ila hawajaona.

Mkondo tofauti wa hekaya za Paul Manyasi, DCI yatoa kauli inayokanganya zaidi

Hekaya za kijana aliyeanguka kutoka kwa ndege nchini Uingereza zinachukua mkondo tofauti siku baada ya siku.

Kwa kile kinachoonekana kama uchunguzi uliogonga mwamba, ofisi ya DCI imetoa kauli kinzani na shirika la habari la Sky News.

Mkuu wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) Bwana Kinoti amesema kuna uwezekano mkubwa kuwa kijana aliyefariki katika ndege ya KQ ,Paul Manyasi ana uraia wa Afrika Kusini.

Katika mahojiano na kituo cha K24, Kinoti amefunguka A-Z kuhusu swala hilo.

(+ Picha )Mke wa Mwanahabari Richard Muema aliyepigwa risasi Kasarani afunguka

“Tungetaka kujua habari zote zinazozingira tukio hili. Aidha ni muhimu tujue kizungumkuti hiki chote kimesababishwa na nini. Tutajitahidi kuona iwapo kijana aliyeanguka kutoka kwa ndege ana uraia wa Kenya ama ni Afrika Kusini…” Kinoti

Kinoti amesema kuwa safari ya ndege hii ilianzia Afrika Kusini kabla itue JKIA.

Taarifa za DCI zinakanganya kwani angepanda ndege Afrika Kusini, mwili wake ungeanguka Kenya punde tu magurudumu yakichomoka.

Wazo la kufikiria kuwa kijana huyu ni raia wa Afrika kusini ni wazo la kupuuzilia mbali.

Haya yanajiri huku sura ya picha iliyochapishwa na Sky News ikifanana na kijana kwa jina Cedric Sivonje.

Inadaiwa kuwa Shivonje amezuiliwa katika jela kwa tuhuma za ubakaji.

Hii ni kulingana na makachero wanaochunguza kisa hiki.

‘Aliyetekwa nyara’ apatikana na mpenzi akijipa raha Thika Road Mall, DCI yaeleza

Idara ya DCI imezidisha juhudi Afrika Kusini kubaini kisa hicho na kudadisi uwezekano wa marehemu kutoka nchi hiyo.

Shirika la habari la Sky News linashikilia kuwa Paul Manyasi ndiye alifariki katika ndege ya KQ.

Ripota wa shirika hili alisafiri hadi Kenya,Kakamega kumhoji anayedhaniwa ‘babake’.

‘Wazazi’ hawa Isaac Beti na Janet walikubali na baadaye wakageuka baada ya kuona habari hizi katika vyombo vya habari.

 

(+ Picha )Mke wa Mwanahabari Richard Muema aliyepigwa risasi Kasarani afunguka

Mwanahabari Richard Muema aliyepigwa risasi kadhaa mwilini anaendelea kupata afueni katika hospitali ya KNH (Kenyatta National Hospital).

Jamaa huyu alipigwa risasi na majambazi wawili waliovamia duka mtaa wa Kasarani viunga vya jiji kuu la Nairobi.

Katika kipande cha video kilichosambaa kama moto wa nyika mitandaoni, Richard alipiga mmoja wa majambazi hao katika juhudi za kuokoa mwenye duka.

rICHARD-MUEMA-WRITER
RICHARD MUEMA

Kitu na ambacho hakujua ni kwamba angepigwa risasi mwilini na kuhatarisha maisha yake.

Fahamu zimemrudia Richard baada ya kupambana na wahuni waliovamia duka Kasarani.

Ugonjwa anaougua Othuol Othuol , namba yatolewa kuchanga hela

Muema alikuwa katika jitihada za kumwokoa muuzaji duka katika video iliyotambaa sana mitandaoni.

Akizungumza na runinga ya Citizen, mkewe alisema kuwa alimtembelea hospitali.

Richard-Muema-KNH
RICHARD MUEMA, wodi ya ICU

Kwa sasa mmewe bado yupo katika sehemu ya watu mahututi wanaohitaji usaidizi wa haraka zaidi.

Aliyetekwa nyara’ apatikana na mpenzi akijipa raha Thika Road Mall, DCI yaeleza

 

Mkewe amesema kuwa anawashukuru zaidi madaktari wa hospitali hiyo.

Familia imejotolea kutoa usaidizi katika hali hii ngumu.

 

Uhuru: Sikudhani uchaguzi wa Kibra ungekuwa wa amani

Rais Uhuru Kenyatta kwa mara ya kwanza amezungumzia kuhusu kushindwa kwa Jubilee katika uchaguzi mdogo wa Kibra.

Jubilee ilikuwa inampigia upato  McDonald Mariga katika uchaguzi huo uliowavutia wagombeaji 24.

Hata hivyo, Mariga alibwagwa na mgombea wa chama cha ODM.

Watu Sita Wauawa Na Umati Katika Kaunti Ya Busia

Uhuru alikiri kwamba Jubilee ilishindwa ila akasema  cha muhimu ni amani uliodumishwa wakati wa kampeni na hata siku ya ukupigaji kura.

“Katika miaka yangu yote sijawai ona kampeni ya amani Kibra. Kuna baadhi ya watu wachache walirushiwa mawe lakini hatukuona duka likichomwa au watu wakiwa na wakati mgumu wakienda nyumbani,” Uhuru alisema.

“Iwapo uchaguzi unaweza ukafanywa Kibra na watu hawatapoteza mali yao au maisha yao basi hiyo ni ushindi na watu wanafaa kujifunza kutokana na hilo,”

Alizungumza hayo katika ikulu ndogo ya Sagana katika kaunti ya Nyeri wakati alipofanya mkutano na wanasiasa kutoka Mlima Kenya.

Rais Uhuru alitoa mfano wa mfuasi wake ambaye kila wakati wa uchaguzi huvamiwa na kutpoteza mali.

Seneta Cleophas Malala Atimuliwa Chamani ANC

Uhuru alisema kuwa kuna mwanamke aliyepotea mali yake katika uchaguzi wa 2007, 2013 na hata 2017 kutoka na vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa uchaguzi.

Alisema kwamba kuwalika watu wengine kujumuik nao haimaanishi kwamba anawafukuza walio karibu na yeye.

Aidha aliwarai viongozi kutoka Mlima Kenya kusahau tofauti zao na kufanya kazi kwa pamoja.

Ugonjwa Anaougua Othuol Othuol , Namba Yatolewa Kuchanga Hela

 

 

 

Watu sita wauawa na umati katika kaunti ya Busia

Watu sita Ijumaa walipigwa hadi kufa na umati uliokuwa na ghadhabu katika kaunti ya Busia.

Sita hao hawakutambuliwa na wenyeji mara moja na wanasemekana  kukodiwa na mwanamke mmoja mfanyabiashara ili kuchukua mwili wa mwanaume mfanyabiashara  aliyekuwa ametekwa nyara na baadaye mwili wake kupatikana katika kijiji cha Marachi.

Seneta Cleophas Malala Atimuliwa Chamani ANC

“Wakaazi waliwashuku walipowaona sita hao wakiwa wamevalia suti nyeusi. Mmoja wao aliyekuwa na begi aliamrishwa kutwaa likaguliwe na ndani yake likapatikana visu vitatu,” kamanda wa polisi kutoka Magharibi Edward Mwamburi alisema.

“Wanakijiji waliwashuku kwamba huenda watu hao walihusika na kifo cha mfanyabiashara huyo na kuwashambulia hadi wakafa.”

Mfanyabiashra John Aduor alitekwa nyara nyumbani kwake Masebula na watu watatu ambapo mmoja wao alikuwa amejihami na bunduki na baadaye Aduor kupatikana ameaga dunia katika Kagonya, kaunti ndogo ya Ugenya.

Kisa hicho kilitokea katika shule ya msingi ya Wamasela ambapo mwili wa mfanyabiashara huyo ulikuwa unatazamwa na umma Ijumaa jioni kabla ya mazishi.

Hafla ya mazishi ilikuwa imepangwa kufanyika Jumamosi katika wadi ya Marachi Magharibi.

Ugonjwa Anaougua Othuol Othuol , Namba Yatolewa Kuchanga Hela

Sita hao wanaaminika kuwa vijana wa kukodiwa na wanasiasa katika Ugenya.

“Tumeanza uchunguzi wetu na yeyote atakayepatikana kutekeleza mauaji hayo atakumbana na mkono wa sheria,” Mwamburi alisema.

Aidha aliwaonya umma dhidi ya kuchukua sheria mikononi mwao.

Orodha Ya Mishahara Ya Waigizaji 10 Bora Ulimwenguni – Forbes

 

 

Seneta Cleophas Malala atimuliwa chamani ANC

Chama cha  Amani National Congress kimefuta jina la Seneta wa Kakamega kutoka sajili.

Kamati ya nidhamu ya ANC ilifikia uamuzi huu Jumatano baada ya kufanya mkutano.

Taarifa kutoka kamati hiyo ya nidhamu inasema kwamba  Malala alimuunga mkono mgombea wa chama cha ODM katika uchaguzi mdogo wa Kibra.

Hii ni kinyume cha katiba na maagizo ya chama hicho.

Rais Mstaafu Mwai Kibaki Aadhimisha Miaka 88 Ya Kuzaliwa

“Baada ya kuchunguza kwa kina, NDC imeamua kuchuku hatua za kinidhamu kwa mwanachama huyo kutoka na sababu kwamba hatua zake zinaenda kinyume na sheria sio ya ANC lakini pia sheria za nchi,” taarifa ilisoma.

Pia taarifa hiyo ilisoma kwamba, “NDC imeamua kumfurusha Cleophas Malala chamani ANC mara moja.”

Katibu mkuu wa ANC Barrack Muluka alisema kwamba Malala ana siku 90 kupinga uamuzi huo wa kamati.

Hata hivyo hatua ya chama hicho kimepingwa na mbunge mteule Godfrey Osotsi.

Osotsi amesema kwamba uamuzi huo ni “utani mkubwa.’

Alisema kwamba  chama cha  ANC kilimteua Eliud Owalo kugombea uchaguzi wa Kibra bila kuwahusisha.

Furaha Kijiji Cha Sobea, Joyce Wairimu Arejea Nyumbani Tangu Vita Vya Uchaguzi

 

 

Ugonjwa anaougua Othuol Othuol , namba yatolewa kuchanga hela

Nyota wa ucheshi nchini Othuol Othuol yupo katika hali sio nzuri kiafya.

Kulingana na taarifa za vyanzo vyetu, Othuol ambaye ni mcheshi katika Churchill show amekuwa akipigana na kifua kikuu kwa kipindi kirefu.

Screenshot_from_2019_11_16_12_22_04__1573897642_82130

Katika mawasiliano ya wacheshi kikundi cha WhatsApp, marafiki wake wanatuma pole zao na kuahidi kutoa usaidizi wanavyoweza.

View this post on Instagram

THANKS FOR WATCHING @churchillshow last night…

A post shared by othuol othuol (@othuol.othuol) on

Kando na kuwa mcheshi Churchill Show, Othuol anahusika katika kipindi cha Aunty Boss.

Aidha, namba ya kutuma usaidizi imesambazwa ili kuchanga hela.

Unaweza ukatuma mchango wako kupitia 0754927977.