Maafisa wa polisi walitumia nguvu isiyo ya kawaida kuingia katika gari lake na kumtia nguvuni mapema asubuhi. Kufikia sasa hakuna taarifa zinazoonyesha aliko Bobi Wine. Waandalizi wa fiesta hii iliyopangiwa ya pasaka ni mojawapo ya watu waliokamatwa katika mchakato huu.
Waandamanaji ambao ni wafuasi wake walipata wakati mgumu waliporushiwa maji yanayowasha mwilini pamoja na gesi ya kutoa machozi katika makabiliano makali na maafisa wa polisi.
Rais wa Uganda Yoweri alikuwa awali amefutilia mbali mikutano katika sehemu za burudani iliyosheheni siasa za kuipinga serikali. Mkali huyu alibaniwa kufanya fiesta na ambalo alikuwa ameiratibisha kuifanya ili kuwakonga nafsi mashabiki wake inayofahamika kama One Love nchini humo.
Wine alikuwa ameita vyombo vya habari kuvihutubia kuhusu kufungiwa kwa tamasha lake na ambalo lilikuwa lifanyike msimu huu wa pasaka pindi alipokamatwa na kupelekwa kusikojulikana.
Robert Kyangulanyi almaarufu kama bobi wine sio mara yake ya kwanza kukamatwa. Baada ya mbunge huyu wa Kyadondo mashariki kukamatwa ,ameonyesha ujasiri kwa wafuasi wake katika mitandao ya kijamii msanii huku akionyesha kutokata tama katika vita dhidi ya utawala katili na wa kidikteta