Bobi Wine kuwa mpizani wake Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi ujao

Mwimbaji wa Uganda, Bobi Wine atakuwa mpizani wake Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi wa 2021.

"Nitakwa mpinzani wake Rais Museveni kwa niaba ya watu," Bobi Wine alisema katika mahojiano na Associated Press news agency siku ya Jumatatu.

Hata hivyo, Bobi Wine alisema kuwa anaswasiwasi juu ya usalama wa maisha yake baada ya kile anachoamini kuwa ni jaribio la kumuua Agosti iliyopita. Dereva wake alipigwa risasi na kuuwawa katika gari lake.

"Ninaishi kila siku bila kuwa na uhakika wa siku inayofuata," alisema nyumbani kwake nje ya mji mkuu wa Kampala. "Mimi sio kipofu na kusema ukweli utawala uliopo unataka mimi nife na nife haraka iwezekanavyo."

 Mwimbaji Jose Chameleone pia ameonyesha hamu katika siasa na amekubali kuunga Bobi Wine mkono.
Soma mengi