Bodi ya nafaka haijawalipa wafanyikazi wake kwa miezi miwili

Wafanyikazi wa bodi ya nafaka NCPB hawajalipwa mishahara kwa miezi miwili iliyopita, afisa wa bodi hio amefichua.

Taasisi hio ya serikali inang'ang'ana kulipa mishahara na bili za umeme.

NCPB inaidai wizara ya kilimo pamoja na hifadhi ya chakula ya kitaifa shilingi bilioni 11.

Afisa huyo ambaye alitaka jina lake kubanwa , amesema hali hio imesababishwa na ufadhili duni kutoka kwa wizara.

Wizara hio inadaiwa shilingi bilioni 8 na NCPB Sh8 ambazo zimekusanyika kutoka mwaka wa fedha wa 2015-16 kutoka kwa ununuzi wa mbolea. Shilingi bilioni 3 zingine zinadaiwa hazina ya chakula, pesa zilizotumika kununua kemikali na mifuko ya kuhifadhi mahindi katika mabohari yao.

Lakini mwenyekiti wa hazina hio Noah Wekesa amekana kudaiwa pesa zozote na NCPB. Badala yake anasema wanaidai bodi hio kwa uuzaji wa mahindi.

“Shida hizo hazituhusu lakini zinatokana na jinsi wanavyoshighulikia masuala yao. Hatuna deni,” Wekesa amesema.

Afisa huyo ameeleza kwamba NCPB hununua mbolea kwa niaba ya wizara ya kilimo.

Mwaka wa 2015-16, NCPB ilichukua mkopo wa shilingi bilioni 4 kununua mbolea na tangu wakati huo kuna salio la shilingi milioni 300. Pia kuna salio la mwaka 2016-17 na 2017-18.

Hii haijumuishi riba mbayo imekusanyika hadi zaidi ya shilingi bilioni 1 na inaendelea kuongezeka,” afisa huyo wa NCPB amesema.

Wekesa anasema bodi hio ni taasisi na jukumu lake ni kununua na kuuza mahindi kulingana na maagizo ya hifadhi ya kitaiga ya chakula.

"Lakini wamekua wakiza mahindi bila ya kutupokeza fedha hizo,”  Wekesa amesema.

Mwenyekiti huyo amesema wataandaa mkutano wa pamoja siku ya alhamisi ili kujadili masuala haya.