Bonge la suprise! Tazama jinsi mashabiki sugu walivyo msherehekea Massawe

Kwa mda wa wiki mzima, mtangazaji wa Bustani la Massawe Japanni, amekuwa akiimba wimbo wa siku yake ya kuzaliwa huku siku yenyewe ikiwa Jumamosi hii.

Katika mtandao wake, Massawe amekuwa akichapisha picha kadha wa kadha za kutoka sherehe zake za birthday zilizopita huku akijitayarisha mwaka huu.

Alipotoka studio siku ya Alhamisi, mashabiki wake sita sugu walimpa bonge la surprise siku mbili kabla ya siku yake ya kuzaliwa.

Mashabiki hao kwa majina; Harriet Omunzi, Chris Ochi, Aida Mwangi,Eric Sugut, Phanice Moraa na Faith Kirimi, walimnunulia keki na glesi za maji na pia kedi murwa ya birthday.

Isitoshe keki waliyomletea ilikuwa imeundwa kiistarabu kwa mtindo wa kisasa ambayo ilikuwa na shepu ya headphones kuashiria taaluma yake ya uanahabari.

Massawe aliyejawa na furaha alichapisha picha zile kwa mtandao wake wa Instagram huku akiwasifu mashabiki wake.

Alisema,

So my ardent fans decided kunipa bonge la surprise two days before my birthday. I'm so humbled by you people , May God bless you and I love you all..Nawalove😘   

Tazama picha zifuatazo.