Boni Khalwale arushiwa mawe na kufurushwa Kibra - Video

Khalwale-compressed
Khalwale-compressed
Seneta wa zamani wa Kakamega Boni Khalwale amefurushwa na wakaazi wa Kibra  alipowasili katika Wadi ya Laini Saba.

Kulingana na video iliyochapishwa kwenye Twitter, Khalwale anaonekana akitoroka makundi ya watu waliokuwa wakimrushia cheche za matusi.

Aidha, watu hao wanaonekana wakirushia mawe kwa Seneta huyo wa zamani.

Baadhi yao walisikika wakisema ""Hapa ni bedroom ya Baba bwana. Hatutaki mchezo"

Kabla ya vurugu hizo, Khalwale alikuwa ametangaza kwenye Twitter kwamba alikuwa katika maeneo ya Kibra.

https://twitter.com/BKhaniri/status/1192347125629227008?s=20

"Deep inside Kibra. Mambo iko bara bara kabisa!"  taarifa kutoka mtandao wake ulisoma.

Masaa chache baada ya kisa hicho, Khalwale aliwahutubia wanahabari kuwa uchaguzi wa Kibra unaendelea vyema ila woga wa ODM unawafanya kutoa malalamishi kuhusu madai ya wapiga kura kuhongwa.

"Tumepiga kampeni ya kutosha ndiyo maana ODM wanatuogopa kinachowapelekea kutoa madai ya rushwa," alisema.

Baadaye Polisi walimwamuru Khalwale kuondoka maeneo hayo.

Awali  Kiongozi wa ODM Raila Odinga amewataka wapiga kura wa Kibra kulinda kura zao katika uchaguzi mdogo unaoendelea.

“Tuko katika chumba chetu cha kulala ‘bedroom’ na nataka kuuliza watu wetu kulinda bedroom yetu dhidi ya watu wa nje,” Raila alisema.

Uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Kibra umevutia jumla ya wagombeaji 24.