Boni Khalwale mashakani baada ya kusema haya kuhusu Joho na Junet

EciWt-fX0AI8odI
EciWt-fX0AI8odI
Aliyekuwa seneta wa kaunti ya Kakamega Boni Khalwale amejipata pabaya baada ya kumkosoa mbunge wa Suna mashariki Junet Mohamed na gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho baada ya kutumia ndege ya kibinafsi na kwenda kumtembelea kinara wa ODM Raila Odinga Dubai.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya twitter, Khalwale alisema kuwa kitendo cha wawili hao kusafiri na ndege hiyo ni kuharibu mali ya umma.

“A private jet just to visit a patient in Dubai. How ua taxes are spent!" Aliandika Khalwale.

Hata hivyo, KOT walimpa bonge la jibu huku wakimkumbusha pia naye alitumia ndege ya kibinafsi kwenda kurekodi habari katika kituo cha polisi cha Kakamega.

Wengine walisema kuwa Khalwale alikuwa amejawa na wivu ndio maana aliandika ujumbe huo usiku badala ya mchana na kumrai angeandika mchana ili wamuone.

Baada ya kuwasili Dubai, wawili hao walipiga picha wakiwa na Baba na kisha kusema walitua nchini humo vyema.

Hizi hapa baaadhi za hisia za wanamitandao;

@JoelGriffine :@KBonimtetezi You didn't need to wait till the dead of the night to tweet. Tweet in broad daylight tukuone

@AmakanjiThomas: @Kbonimtetezi You forget so quickly when you took a chopper to kakamega just to appear for the summonThinking face you and #WetaTheRutoProject are similar. How much did it cost?

Naye Gavana Joho hakuachwa nyuma bali alikuwa na haya ya kusema;

“Delighted to see my party leader Baba @RailaOdinga looking fit and in high spirits after undergoing the surgical procedure in Dubai last week. We in Mombasa and the country at large continue to pray for his speedy recovery and a safe return home to Kenya. @JunetMohamed”