Boni Khalwale aomba rais kusitisha utumizi wa noti mzee

Aliyekuwa seneta wa Kakamega Boni Khalwale amemtaka Rais Kenyatta kusitisha utumizi wa noti mzee hivi sasa iwapo lengo la kuzindua noti mpya ni kukabili ufisadi

Khalwale amesema haina haja kusongeza muda mbele na kupeana nafasi kwa wafisadi walio na noti mze kujipanga.

Kwingineko

Wazee wa jamii na viongozi wa kidini wameshauriwa kuingilia kati swala la dhulma za kijinsia kwa kutoa ushauri kwa jamii ili kupunguza visa hivyo.

Mwakilishi wa kike kaunti ya Taita Taveta Lydia Haika anasema endapo wazee katika jamii na viongozi wa kidini wataeneza hamasa dhidi ya dhulma za kijinsia, huenda visa vya mauaji vinavyoripotiwa kwa sasa vikaoungua.

Kwingineko

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya mazingira, shule moja huko Wundanyi kaunti ya Taita Taveta imejizolea sifa kwa kutumia gesi ya biogas kupikia badala ya kuni katika juhudi za kukabili uchafuzi wa hewa.

Mwalimu mkuu wa shule ya wasichana ya Senior Chief Mwangeka, Christine Mlemwa anasema tangu kuanzishwa kwa mtambo huo wa gesi mwaka jana, shule hiyo imepunguziwa mzigo wa kununua kuni huku bakshishi inayosalia katika tanki la gesi ikitumika pia kama mbolea katika shamba la shule.

Wanafunzi shuleni humo aidha, wamesifia mradi huo wakisema wanautumia pia kwa somo la kemia na kilimo na kuzishawishi taasisi zingine za elimu kukumbatia mbinu hiyo inayolinda mazingira.