Nchi ya Botswana imefutilia mbali sheria ya enzi za ukoloni iliyoharamisha mapenzi ya jinsia moja katika kesi kubwa iliyokuwa ikifuatiliwa na watu wengi barani afrika .
Uamuzi huo wa Botswana unajiri siku chache tu baada ya Kenya hivi maajuzi kutilia mkazo msimamo wa kuharamisha mapenzi ya jinsia moja .
Mahakama kuu jijini Gaborone imesema sheria iliyokuwa ikitoa adhabu kali kwa ushoga na mapenzi ya jinsia moja wa jumla ilikuwa kinyume na katiba .