Brazil kukambana koo na Peru kwenye fainali za Copa America

Peru iligaragaza Chile magoli matatu bila jibu  hivyo kuibandua kwenye nusu fainali ya pili ya Copa America. Edison Flores aliwaduwaza Chile kunako dakika ya 21 baada ya kukamilisha krosi yake Andre Carrillo.

Chile walitawaza mchezo jambo lililowafanya kuiacha gome yao ya ulizi ikisuwasuwa.

Makosa ya mlinda lango Gabriel Arias yaliadhibiwa na Yoshimar Yotun kunako dakika ya 38. Kipindi cha pili Peru walikamilisha maneno kupitia nahodha wao Paulo Guerrero alipocheka na wavu dakika 91.

Kufuatia ushindi huo sasa Peru itavaana na Brazil katika fainali tarehe 7 huku Chile ikikipiga dhidi ya Argentina kwenye kuwania nafasi ya tatu mnamo tarehe 6.

Kwingineko, U.S.A itamenyana na mexico kwenye fainali za CONCACAF tarehe nane. Ikiongozwa na mshamulizi wa Chelsea, Christian Pulisic, U.S.A ilicharaza Jamaica 3-1 kwenye nusu fainali ya pili.