Brazil yatwaa taji la Copa America

Brazil ilitawazwa mabingwa wa Copa America baada ya Kuicharaza Peru 3-1. Everton aliipa Brzail uongozi mnamo dakika ya kumi na tano. Peru ilisawazisha mnamo dakika ya 44  kupitia tuta la penalti baada ya Thiago Silva kunawa mpira.

Gabriel Jesus aliipa Selecao uongozi kabla ya kipindi cha kwanza kuisha akikamilisha pasi kutoka kwake Roberto Firmino.Richarlison alitia kimiani goli la mwisho kwenye michuano hio mnamo dakika ya 89 kupitia njia ya penalti.

Brazil ilitawazwa mabingwa wa Copa America baada ya Kuicharaza Peru 3-1. Everton aliipa Brzail uongozi mnamo dakika ya kumi na tano

Dani Alves alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano huku Alisson Becker akichaguliwa kuwa mlinda lango bora.

Kwingineko ni kuwa Mexico ilitwaa taji la CONCACAF gold baada ya kuigaragaza U.S.A goli moja bila jibu. Jonathan Dos Santos alifunga goli la kipekee la mchezo kunko dakika ya 73.