Am broke! Sonko adai hawezi kuwajibikia familia yake baada ya akaunti zote kufungwa

Gavana wa Nairobi Mike Sonko sasa amedai kuwa hawezi kujukumikia familia yake kama mzazi kutokana na hatua ya serikali kuzifunga akaunti zake zote. Kupitia kwa wakili wake Harrison Kinyanjui, Sonko anataka maamulizo yaliyotolewa mnamo Februari 6 mwaka huu kumruhusu kupokea mshahara wake ili aweze kuikimu familia yake.

Febrauri 6,  jaji Luka Kimaru alizifunga akaunti 10 zilikuwa zinamilikiwa na kiongozi huyo na ambazo zilikuwa zimetumika kuweka milioni 8 za wizi kutoka kwa kaunti ya Nairobi.

Pesa hizo ziliwekwa katika benki tofauti ikiwemo Equity, Diamond Trust na Cooperative bank. Agizo hilo liliotolewa baad ya mamlaka ya kurudisha mali ya serikali almaarufu kama Assets Recovery Agency kusema inashuku kuwa pesa hizo zilitumwa kwa benki hizo na zingine kutolewa mnamo mwaka 2017 na 2019.

Japo Sonko kwa upande wake amesema kuwa mamlaka hiyo haikutoa ushahidi wa kutosha wa kuonyesha kuwa aliweka pesa hizo kwa akaunti hizo katika miaka hiyo inayodaiwa.

“The agency did not furnish the court with any compelling grounds or proof to raise reasonable suspicion with respect to any fraudulent transaction related to his bank accounts in question. It only made unsubstantiated claims,” amesema Sonko.

Sonko pia analalama kuwa uamuzi uliofanywa na jaji Kimaru hauwezi kuendelea kutumika hata baada ya siku 14 huku akiishtumu mamlaka hiyo kwa kuendelea kuzifunga akaunti hizo.

Amesema hakuwa gavana wakati ambapo mamlaka hiyo inadai aliipa milioni hizo .

“It is not enough for the Agency to merely make allegations based on wild unspecified suspicions. I believe that the burden of proof lies with them to make out a strong case based on verifiable facts,” amesema Sonko.

Kwa sasa, anataka kesi hiyo kurudishwa kwa jaiji Kimaru ambaye alitoa uamuzi wa kwanza wa kuzifunga akaunti hizo zote ili aweza kuuangazia upya.

“I've never received any summons, telephone call or even a request in writing by the agency to date, to explain any deposit, withdrawal, transfer or transaction of the frozen accounts,”alisema.