Bunduki,14 ,zapatikana katika mkutano wa kaunti ya Nairobi

Waziri wa usalama wa ndani Fred Matang'i  alikashifu  vurugu na vita ambavyo vilitokea katika mkutano wa kaunti ya Nairobi mnamo jumatano, huku mwakilishi wadi Patricia Mutheu akiachwa na majeraha.

Huku akizungumza Jumanne, Matiang'i alisema kuwa bunduki,14, zilipatikana katika mkutano wa kaunti hiyo na kusema limekuwa eneo la vita huku majangili wakiathirika mwishoni.

Matiang'i alisema kuwa atauliza ushauri kutoka kwa baraza la usalama wa kitaifa, pia alikashifu kitendo ambacho polisi walikifanya katika eneo la City Hall jumanne wiki hii.

Haya yanajiri saa chache baada ya wawakilishi wadi kuzua vurugu na kujilazimisha kuingia katika mkutano wa kaunti ya Nairobi ili kumtimua spika Beatrice Elachi kwenye kiti chake.

Polisi waliwazuia wawakilishi wadi huku wakizua vurugu na vita kushuhudiwa  baina ya polisi na wawakilishi wadi.

Polisi hao walilazimika kutumia vitoa machozi ili kuwatawanyisha wawakilishi wadi hao, video ya polisi hao na wawakilishi wadi ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii na hata kuzua gumzo kwenye mitaandao hiyo.

maafisa wa polise,4, walionekana kutumia nguvu zao na hata kutumia ruungu huku wakimcharaza MCA Patricia Mutheu huku akiomba kuonewa huruma.