Ali alikuwa miongoni mwa washirika 16 wa naibu wa rais William Ruto kupigwa shoka kutoka kamati za bunge mwezi jana na mageuzi yaliyoendeshwa na rais Uhuru Kenyatta . Mbunge huyo wa Moiben alichaguliwa bila kupingwa siku ya alhamisi .
Mwakilishi wa akina mama wa Laikipia Catherine Waruguru alichaguliwa kuwa naibu mwenyekiti wa kamati hiyo .anaichukua nafasi ya mbunge wa Navakholo Emmanuel Wangwe, aliyeteuliwa kuwa kiranja .Tiren anaichukua nafasi hiyo alioyolazimika kuiacha baada ya Chama cha Jubilee kumpendelea Ali mwaka wa 2018.
Mbunge wa Shinyalu Justus Kizito na mwakilishi wa akina mama wa Nyamira Jerusha Momanyi walichaguliwa kuwa mwenyekiti na naibu mwenyekiti wa kamati ya matangazo na makataba .walichaguliwa bila kupingwa .mbunge wa Limuru Peter Mwathi na mwenzake wa chepalungu Gideon Koske watahudumu katika kamati ya bunge kuhusu leba na huduma za kijamii kama mwenyekiti na naibu wake mtawalia .
Upande wa walio wengi na wachache tayari zimekubaliana kuhusu uongozi wa kamati mbali mbali na uchaguzi utakuwa tu kama njia rasmi ya kuidhinisha mwafaka huo . Kwa mfano mwakilishi wa akina mama wa Homabay Gladys Wanga amependekezwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango na naibu wake atakuwa mbunge wa Roysambu Waihenya Ndirangu