BUNGOMA: Afisa Wa KDF Ajiua Baada Ya Kuua Mwanawe Wa Miaka Miwili

Hali ya huzuni imetanda katika kijiji cha Makunga kata ya Mbakalo eneo bunge la Tongareni kaunti ya Bungoma baada ya afisa mmoja wa KDF kudaiwa kumuua kwa kumdunga kwa kisu mwanawe wa umri wa miaka miwili kabla ya kujitoa uhai pia kwa kujidunga kwa kisu tumboni.

Kulingana na majirani ni kuwa mwendazake alijifungia chumbani mwake akiwa amemteka nyara mwanawe mchanga akitishia kumuua kwa kisu na kujiua pia kwa kile kinachoaminiika kukosa imani na mkewe ambaye alikuwa amesafiri jijini Nairobi wakati wa kisa hicho.

Hata hivyo, wakaazi wa eneo hilo wamewalaumu maafisa wa polisi kwa kuchelewa kufika eneo la tukio mapema ili kumunusuru mtoto huyo mchanga.

-Brian Ojamaa