crime

BUNGOMA: Mtahiniwa Wa Kidato Cha Nne Afariki Hospitalini

Mtahiniwa mmoja wa kidato cha nne kutoka shule ya upili ya Mabusi eneo bunge la kanduyi kaunti ya Bungoma amefariki mapema leo katika hospitali ya rufaa ya Bungoma.

Kellen Wanyonyi Nekesa mwenye umri wa miaka 22 alifariki muda mchache kabla ya kuanza mtihani wake aliokua akifanyia katika hospitali hio.

Afisa mkuu wa matibabu katika hospitali hio Mayama Magrina amesema kwamba mwanafunzi huyo aliyefikishwa katika hospitali hio siku ya jumapili usiku heunda alifariki kutokana na ugonjwa wa (Septicemia) bacteria mingi katika mwili wake.

Babake mwendazake Justus Wanyonyi amesema kwamba ni jambo la kutamausha mno kutokana na kifo cha mwanawe ambaye alikua ni tegemeo kwa siku za usoni.

Aidha amesema huenda msichana huyo alifariki kwa kutaka kuavya mimba kutokana na madawa ya kienyeji anayosemekana alipewa baada ya kugundua ni mja mzito.

-Brian Ojamaa

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments