BUNGOMA: Polisi walaumiwa kufuatia kifo cha kutatanisha

Photo source: kenyacarbazaar.com

Mwakilishi wa wadi ya Soysambu Mitua eneo bunge la Tongaren Kaunti ya Bungoma Gershom Namasake amewalaumu pakubwa maafisa wa polisi wa kituo cha Soysambu kwa kifo cha kijana mmoja kutoka eneo hilo aliyejitoza majini katika mto Nzoia akiwa na pingu mikononi.

Akiongea katika kikao na wanahabari mjini Webuye Namasake amesema kuwa maafisa hao walimtesa na kuumiza marehemu mwenye umri wa miaka ishirini na nne bila kosa kwani pesa anazolaumiwa kuiba alizipata kutoka kwa rafikiye.

Namasake amedai kuwa maafisa hao hawakuwa na kibali cha kumkamata kijana huyo ambaye alipatikana amefariki majini baada ya siku tatu.