BUNGOMA: Shangwe Na Nderemeo Baada Ya Wycliffe Wangamati Kutangazwa Gavana Mpya

wangamati
wangamati
Kulikua na sherehe na nderemo jana usiku kucha katika boma la mgombea kiti cha ugavana kwa tikiti ya chama cha Ford Kenya, Wycliffe Wangamati ambaye alitangazwa rasmi hapo jana kama gavana wa Bungoma baada ya kumbwaga gavana ken Lusaka.

Wangamati amewashukuru wakaazi kwa kumpa fursa kuwa gavana wa pili wa jimbo la bungoma na kuahidi kuwatumikia wakaazi kuafikia maendeleo ipasavyo.

Seneta wa Bungoma Moses Wetangula amepongeza ushindi huo na kusema kwamba chama cha Ford Kenya kitashirikina na Wangamati ili kurejesha hadhi njema ya kaunti hio iliyoptezwa na gavana Lusaka.

Kwingineko, Danson Mwashako wa chama cha Wiper ndiye mbunge mpya wa Wundanyi.

Mwashako amekitwaa kiti hicho kwa kura 8,373 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Simon Mwachia wa Jubilee aliyepata kura 5, 116. Cromwell Baridi wa Ford Kenya alimaliza wa tatu kwa kura 2,864.

-ojamaa